UHURU WA WANAHABARI KATIKA UTENDAKAZI WAO WATILIWA SHAKA

Mshirikishi wa shirika la wanahabari la (KCA) ukanda wa Pwani Baya Kitsao amesema uhuru wa wanahabari, bado haujakubainika kikamilifu humu nchini, na ulimwenguni kwa Jumla.
Kulingana na Baya kumekuwa kukishuhudiwa ongezeko la visa vya ukosefu wa usalama wa wanahabari ulimwenguni, ikiwemo kupigwa na hata wengine kuuwawa.
Akizungumza na wanahabari mjini kilifi Baya amesema, wanahabari ni viungo muhimu Katika jamii, na wanapaswa kuwa huru na usalama wao kulindwa wakati ambapo wanatekeleza majukumu yao.
Wakati uo huo ameiomba Idara ya upelelezi kufanyia uchunguzi kesi za wanahabari waliouwawa Katika hali tatanishi, ili waweze kupata haki.
Baya hata hivyo amegusia swala la wanahabari wengi kuachishwa kazi kiholela, na kuzitaka Idara husika kutowaachisha kazi wanahabari hususan kipindi hiki kigumu.
Haya yanajiri huku ulimwengu ukiadhimisha siku ya uhuru wa wanahabari duniani hapo jana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.