UCL | Suarez ageuka sumu kwa Inter Milan, aisaidia Barca kupata ushindi wa 2-1

Mshambuliaji wa kimataifa wa Uruguay anayeichezea FC Barcelona ya Hispania Luis Suarez, usiku wa tarehe 2 Oktoba 2019 katika uwanja wa Nou Camp aliibuka shujaa wa mchezo dhidi ya Inter Milan katika UEFA Champions League hatua ya makundi baada ya kuwatoa kijasho chembamba wapinzani wake kwa mabao 2-1.

Barcelona baada ya kurudi katika uwanja wao wa Nou Camp walianza vibaya kwa kujikuta wakiruhusu kufungwa goli la mapema na Inter Milan dakika ya pili kupitia kwa Lautaro Martinez lakini mambo hayakuwa mazuri kwa Barcelona hadi walivyoingia kipindi cha pili.

Luis Suarez alikuwa mkuki wa sumu wa Inter Milan kwani alifunga goli la kusawazisha dakika ya 58 na kufunga goli la ushindi dakika ya 85 na kuufanya mchezo umalizike kwa Barcelona kupata ushindi wa 2-1, Lionel Messi akiibuka kidedea kwa kutengeneza nafasi nyingi zaidi (6) kuliko mchezaji yeyote katika mchezo huo,

Barcelona sasa wapo nafasi ya pili kwa kuwa na point 4 katika kundi lao sawa na Dortmund inayoongoza wakati Inter Milan na Slavia Prague wakiwa na point moja moja kila mmoja.

Aidha kwenye mechi nyengine za michuano hiyo ni kuwa Liverpool wameandikisha ushindi wa 4-3 dhidi ya Red Bull Salzburg huku Chelsea wakivuna ushindi wa 2-1 mikononi mwa Lille Olympique.

Ajax wameibamiza Valencia magoli 3 bila jawabu, Zenit ikiwalima Benfica magoli 3-1 wakati RB LeipZig ikilalia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Lyon.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.