UCL | MICHUANO YA KLABU BINGWA KUANZA RASMI LEO

Sasa ni rasmi, Chelsea kuliweka mezani kombe la Ligi ya Mabingwa na kuianza safari ya kulitetea. Ataweza au miamba mingine ya Ulaya italitwaa? Safari ya mabingwa inaanza hivi;

FC Barcelona kuwaalika Bayern Munich katika mchezo wa kwanza wa Kundi E. Barca hii ni muoenekano mpya wa kikosi ambacho hakina Lionel Messi, shujaa wao aliyetwaa tuzo 6 za Balon d’Or akiwa na BarcelonaBayern nao wataingia wakiwa na machungu ya kupoteza ubingwa msimu uliopita. Hakika, ni burudani ya kibingwa.

Young Boys watakua uwanjani kuwaalika Manchester United kule Switzerland. CR7 ndani ya kikosi cha The Red Devils, akiipeperusha bendera nyekundu kwa mara ya pili baada ya miaka 12.

Jumatano, Atletico Madrid watawaalika FC Porto ndani ya Wanda Metropolitano katika mchezo wa Kundi B. Timu zote zinahistoria nzuri na mashindano haya na lolote linaweza kutokea ndani ya uwanja.

Liverpool watakua Anfield kumualika Zlatan Ibrahimovic na wenzake wa AC Milan. Sasa hii ndio vita ya watu wazima, timu hizi ni miongoni mwa miamba ya soka la Ulaya. Mpira wa kistaarabu lakini upinzani wake ni mkali sana!

 Alhamisi kutapigwa mchezo wa Ligi ya EuropaCrvena Zvezds vs Braga kunogesha siku yako.

 

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.