TEDDY MWAMBIRE AMEAPA ATAKAYEIDHINISHWA NA GAVANA KINGI ANASHINDWA KWENYE UCHAGUZI

Nitahakikisha kiongozi atakayeidhinishwa na gavana  wa Kilifi Amason Kingi kuwania wadhifa wa ugavana kaunti ya Kilifi anashindwa wakati wa uchaguzi mkuu ujao wa mwaka wa 2022.
Ni kauli ya Mbunge wa Ganze kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire ambaye amesema  Gavana Kingi hafai kuwaidhinishia wenyeji atakayewania wadhifa huo na badala yake kuwaachia wakazi wa kaunti ya Kilifi kujichagulia kiongozi ambaye  wanaona atawafaa katika kuwaongoza na kuwatekelezea maendeleo .
Akizungumza katika eneo bunge lake , Mwambire anadai Gavana Kingi ana njama fiche ya kumteua mgombea wa  kiti hicho, kauli ambayo  imeungwa mkono na kiongozi wa vijana wa kaunti ya Kilifi  Fikiri Jacobs ambaye pia aliweka wazi  azima yake ya kuwania kiti cha Useneta kaunti ya Kilifi .

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.