Tana River | Vijana wahimizwa kutojiunga na makundi ya kigaidi

Shinikizo linazidi kutolewa kwa vijana kujiepusha kujiunga na makundi ya kigaidi kwa madai ya ukosefu wa kazi.

Akitoa shinikizo hilo kiongozi wa vijana katika kaunti ya Tana River Mohamed Argamso amewataka vijana kuhakikisha wanatafuta mbinu mbadala za kujiendeleza maishani ili kupeukana na vishawishi vya kujiunga na mambo maovu.

Kwenye mkutano ambao uliandaliwa katika shule ya msingi ya Hola uliowaleta pamoja maafisa wa serikali na vijana wa kaunti hiyo ni kuwa wengi wao wamelalamikia swala la mihadarati, ukosefu wa kazi sambamba na elimu duni.

Wakati uo huo Solomo Adhe ambaye ni mwenyekiti wa kundi la Sauti ya Vijana kaunti hiyo amewataka vijana hao kukumbatia elimu kwani kando na kuwa hawana ajira idadi kubwa haina stakabadhi hitajika.

Hata hivyo Abbas Kunyo ambaye ni waziri wa maswala ya vijana katika kaunti hiyo ya Tana River amesema serikali imeweka mikakati kuhakikisha inawasaidia vijana ili kuwasaidia kujiendeleza maishani na kuwaepusha kujiunga na makundi ya kihalifu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.