TAIRENI NA WAZEE WA KAYA WAKONGAMANA

Muungano wa Mijikenda wa Taireni na wazee wa Kaya wamekongamana  kujadili jinsi ya kutetea haki za wakaazi wa ukanda wa pwani.

Kongamano hilo limejumuisha Wazee wa kaya lengo kuu likiwa ni kuhakikisha kuwa wapwani wanafaidika kupitia raslimali zilizopo ukanda huu.

Mwenyekiti wa muungano huo,Peter Ponda amesema kuwa ni wakati sasa wapwani kuungana ili kutetea haki zao zinazohujumiwa miaka nenda miaka rudi.

Kwa upande wake mratibu wa wazee wa kaya Tsuma Nzai, anasema ushirikiano huo unalenga kuleta matumaini mapya kwa wananchi ambao wamekuwa wakiteseka, bila maslahi yao kuangaziwa sawa na kusaidia kupigania haki kwa kufuata sheria ili kuboresha maisha ya vizazi vijavyo.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.