STARTIMES YAJIONDOA KWENYE DILI NA FKF

Kampuni ya utangazaji ya malipo ya televisheni ya StarTimes imetangaza kusitisha mkataba wao wa shilingi milioni 110  ka mwaka na shirikisho la soka la kenya.

Mkataba huo wa haki za matangazo wa miaka saba uliotiwa saini mnamo November mwaka jana umekuwepo kwa mwaka mmoja peke yake.

Katika taarifa startimes iliorodhesha sababu zilizolazimisha kughairi mkataba huo huku ikishtumu FKF iliyovunjwa kwa kutekeleza vibaya makubaliano yao.

Maendeleo hayo ni hatua kuu ya hivi punde zaidi ya kujiondoa kuwa mshirika wa kibiashara na FKF kufuatia ule wa kampuni ya bahati nasibu ya BetKing ya Nigeria ambayo ilisitisha mkataba wao bilioni 1.2 miezi mitatu iliyopita.

Dili hilo la Startimes awali liliwezesha matangazo ya ligi za juu humu nchini, mechi za kirafiki za timu ya Taifa ya Harambee Stars pamoja na mechi 30 za National Super League.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.