SOGORA WA WIKI : RUSSEL CARRINGTON WILSON

Wacheni Watoto wadogo waje kwangu kwa maana ufalme wa mbinguni ni wao.

Maneno yake yesu kristu akiwa duniani wakati Watoto walikuwa wanabanwa kumuona yeye.

Siku zote ni furaha ya mzazi kumuona mtoto wake akiwa mzima na hiyo ndio raha ya jamii.

Russel Carrington willson anayeiwajibikia Denver Broncos ni mchezaji wa American football quarteback, katika ligi ya kitaifa  NFL  na amejitwika jukumu la kuwa shujaa wa afya za Watoto nchini Marekani.

Willson mzawa wa novemba 29 mwaka 1988 nchini marekani, alianza safari yake katika tasnia ya michezo mwaka 2008 akiwa mwanafunzi katika chuo kikuu na hadi sasa  amecheza katika timu kubwa nchini marekanikama vile Tri city dust na NC state.

Mwaka 2012 aliteuliwa na klabu maarufu seattle seanawks  ambapo katika msimu wake wa kwanza alifanya vizuri Zaidi na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa msimu maarufu NFL rookie of the year.

Vile vile aliisaidia timu hiyo yake ya seattle seanawks   kunyakua mataji mawili  makubwa nchini marekani katika ligi ya kitaifa NFL maarufu super bowl.

Aidha pia anashikilia rekodi ya kushinda mechi nyingi Zaidi kama quarterback, katika historia ya nfl.

Wilson ambaye ni mmoja kati ya wamiliki wa klabu ya seatle sounders inayoshiriki ligi ya MLS yaani Major League Soccer, ni mdhamini wa kujitolea katika jamii ya seattle maarufu seattle community inayotoa usaidizi kwa jamii haswa jamii ya Watoto nchini marekani. Angalau kila wiki Wilson hutenga mud ana kuwatembelea Watoto hospitalini seattle iliyo chini ya wakfu wa  why not you  ambao unawasaidia Watoto walio na ugonjwa wa saratani.

Wilson hushiriki katika kuchangisha fedha zinazoenda katika mashirika ya kufaidi jamii, pia akiandaa mashindano ya mchezo wa soka katika miji tofauti tofauti nchini marekani kwa ajili ya kampeni dhidi ya ugonjwa kisukari chini ya mwavuli wa Charles ray (iii) diabetis association shirika ambalo yeye ndiye balozi wa kitaifa nchini humo.

Wilson pia ameshiriki katika kampeni nyingi katika jamii kama vile za kupiga vita dhidi ya ugonjwa wa saratani, lakini pia katika kampeni za kugawa chakula  kwa watu wenye uhitaji haswa wakati wa janga la Korona.

Ni Dhahiri kuwa Wilson sio tu mchezaji ugani bali pia ni mwanadamu wa kawaida mwenye kuelewa changamoto za Maisha. Ugani aking’ang’ana kunyakua ushindi, duniani pia anajitahidi kuyapiku majanga kama njaa na saratani. Je Rafiki, kando na shida zako, ushaiwaza kumtatulia mwenzako pia anayekumbwa nazo? Siku zote haijalishi ni nani wapi lini au nini kusimama kwa zamu haitegemei hali tukumbukane njiani tusipitane shidani.

Tusimwachie msamaria mwema anyakue baraka za kusaidia wakati tunawaacha na kuwatenga walio wa kwetu.

Waswahili walisema kutoa ni moyo usambe ni utajiri, bila shaka hatuwezi kusaidia kila mmoja bali kila mmoja anaweza kusaidia kila mmoja.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.