SHIRIKA LA MSALABA MWEKUNDU LAUNGA KUTANGAZWA KWA UKAME KAMA JANGA LA KAITAIFA

Katibu mkuu wa shirika la Msalaba Mwekundu nchini Daktari Asha Mohammed amesema wanaunga mkono hatua ya rais Uhuru Kenyatta kutangaza ukame kuwa janga la kitaifa.
Asha amesema wameunga mkono hatua hiyo kufuatia utafiti wao kuhusiana na kiangazi ambacho kilibaini kuwa kuna haja ya mikakati ya haraka kuidhinishwa kwa kile ambacho anakisema idadi kubwa ya Wakenya wako hatarini kuaga dunia kutokana na baa la njaa.
Kwa mujibu wa shirika hilo idadi ya watu ambao waliathirika kutokana na kiangazi imeaongezeka kutoka watu milioni 1.4 mnamo mwezi Machi mwaka huu wa 2021 hadi Milioni 2 kwa sasa.
Aidha amesema huenda idadi hiyo ikaongezeka hadi milioni 3 ifikapo mwezi Desemba mwaka huu huku hazina ya kitaifa ikiwa tayari imetangaza kuwa leo itatoa shilingi bilioni 2 ambazo zitatumika kugharamia miradi ya kukabiliana na kiangazi katika kaunti ambazo zimeathirika.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.