SHIPETA AIUNGA MKONO MAHAKAMA

Baadhi ya wanaharakati wa haki za kutetea haki za kibinadamu kaunti ya Mombasa wamesema kuwa hatua ya mahakama kutoidhinisha sheria ambayo inahitaji wagombea kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2022 kuwa na shahada ni afueni kwa vijana ambao wanapania kujiingiza kwenye siasa.
Wanaharakati hao wakiongozwa na Afisa wa Masuala ya dharura katika shirika la kutetea haki za kibinadamu nchini la Haki Africa Mathius Shipeta ambaye ametangaza nia ya kuwania wadhifa wa uwakilishi wa wadi eneo la Mikindani amesema vijana wengi hawakubahatika kupata elimu ya juu na iwapo sheria hiyo ingepitishwa idadi kubwa ingekosa nafasi za kuwania uongozi nchini.
Hata hivyo amesema kuwa ni haki ya kila Mkenya kuwania wadhifa wowote nchini.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *