Shilingi milioni 200 kutumika kukidhi mahitaji ya familia zisizojiweza Mombasa

Kima cha shilingi milioni 200 zimetengwa na serikali ya kaunti ya Mombasa ili kukidhi mahitaji ya familia zisizojiweza endapo marufuku ya kutotoka nje yatatekelezwa kikamilifu.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari gavana wa kaunti hiyo Ali Hassan Joho amesema kila mwenyeji wa kaunti hiyo atasambaziwa kiwango Fulani cha fedha kukidhi mahitaji.
Wakati uo huo ameongeza ili kuafikia hilo kamati maalum inayojumuisha sekta ya binafsi imebuniwa huku akiwahimiza wahisani kujitokeza ili kutoa msaada wa chakula katika shule ya msingi ya Tom Mboya ambayo kwa sasa imetengwa rasmi kwa minajili ya ukusanyaji wa chakula.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.