SERIKALI YA KWALE KUANDAA KIKAO NA KAMPUNI YA BASE TITANIUM PAMOJA NA WENYEJI WA MAFISINI

Serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Base Titanium inapania kufanya mazungumzo na wenyeji wa Mafisini kule Msambweni ili kutatua mzozo uliopo kwa sasa baada ya wenyeji hao kudinda kuchukua fidia ya laki tatu kwa kila ekari ya mashamba yao.

Kufuatia mvutano kutokana na fidia hiyo serikali imebainisha kuwa itawaunganisha wakaazi wa Mafisini sambamba na wakurugenzi wa kampuni hiyo ili kupata mwafaka wa swala hilo.

Ni kauli iliyoungwa mkono na naibu kamishna kaunti ya Kwale, James Kosgey ambaye amesema kuwa harakati za kutanzua utata huo zinapaniwa kutekelezwa ili kupata suluhu kwa wakati ufaao.

Aidha wakaazi wa eneo hilo wamependekeza kupewa kima cha shilingi milioni 15 kwa kila ekari moja ya mashamba kwa kile walichokisema kuwa mashamba hayo yanawingi wa mimea wanayotumia kujikimu hivyo kutolewa kwao katika mashamba hayo kutawaathiri pakubwa.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.