SERIKALI YA KAUNTI YA TAITA TAVETA YA ZINDUA KITUO CHA KUTENGENEZA GESI OXIGENI

Serikali ya kaunti ya taita Taveta imezindua rasmi kituo cha kutengeneza gasi ya Oksijeni, katika hospitali ya rufaa ya Moi katika kaunti hiyo.

Akizungumza katika kituo hicho naibu gavana wa kaunti hiyo Majala Mlaghui amesema kuwa, hatua hiyo ya kuzinduliwa kwa kituo hicho itasaidia pakubwa katika kupunguza gharama za kusafirisha oxegeni, kutoka kaunti ya Mombasa na hata maeneo mengine ya taifa hili, na kuwasaidia wagonjwa wa virusi vya korona na maradhi mengine katika eneo hilo.

Hata hivyo Majala ameongeza kuwa serikali ya kaunti hiyo imeendelea kujitahidi, katika kuboresha hudumu za afya eneo hilo, hasa katika hospitali ya rufaa ya Moi mjini Voi kwa kuhakikisha kuwa wanaongeza vifaa vya kusadia wagonjwa mahututi.

Aidha ametoa wito kwa wakaazi wa kaunti hiyo kutilia maanani maagizo ya wizara ya afya, ili kuona kwamba wanaepuka kupata maambukizi ya maradhi ya covid 19.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.