SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA YA TAKIWA KUTENGENEZA MABOMBA YA KUPITISHIA MAJI CHAFU MJINI..

Serikali ya kaunti ya Mombasa imetakiwa kuchukua tahadhari ya haraka wakati huu wa majira ya mvua, kuzibua mabomba ya maji taka ili waweze kuepuka mafuriko katika maeneo mbali mbali ya mji.

Akiongea na wanahabari mwanaharakati Ben Oluoch amehoji kuwa kuna baadhi ya maeneo, ambapo takataka ziko kandoni mwa mabomba ya kupitisha maji na kuitaka serikali ya kaunti hiyo, kuchukua hatua ya kuondoa taka hizo.

Oluoch amewahimiza wananchi kujikakamua kuona kwamba, wanaondoa takataka zilizoko karibu na nyumba zao, kwa ajili ya kupunguza mbu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.