SEKTA YA UVUVI YATARAJIWA KUIMARIKA

Mikakati zaidi imewekwa na wizara ya kilimo na uvuvi ukanda wa pwani ili kukabiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikiikumba sekta ya uvuvi.
Akizungumza katika ziara ya kufuatilia miradi ya kitaifa ya maendeleo kwenye idara ya uvuvi na masuala ya baharini mwenyekiti wa kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa nchini ambaye pia ni Mbunge wa Moiben Silas Kipkoech Tiren amesema kamati hiyo itakuwa ukanda wa pwani ili kufuatilia miradi ambayo inapaswa kutekelezwa na ni jinsi gani baadhi ya viwanda vitaweza kufufuliwa kuinua uchumi.
Kwa upande wake Mbunge wa mvita kaunti ya Mombasa Abdulswamad sharif Nassir ambaye aliandamana na kamati hiyo amesema kuna changamoto nyingi katika idara hiyo ambazo zinapaswa kutiliwa maanani ili kuiboresha.
Kamati hiyo imeratibiwa kukita kambi ukanda wa pwani kwa muda wa wiki moja ili kukagua miradi tofauti katika kaunti ya Mombasa, kilifi na kwale.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.