SEKTA YA UTALII KAUNTI YA KWALE YATARAJIWA KUANZA KUIMARIKA

Washikadau katika sekta ya utalii wameeleza matumaini ya kuimarika kwa sekta hiyo hata zaidi katika eneo la Diani kaunti ya Kwale.

Washikadau hao wamesema kufikia sasa zaidi ya asilimia 40 ya watalii wamekuwa wakizuru mji huo wa kitalii  katika hoteli mbalimbali licha ya kuwa bado kunashuhudiwa msambao wa virus vya Corona.

Aidha wamesema kuwa wamekadiria kufikia asilimia 70  ya watalii ifikapo mwezi disemba

Wameongeza kuwa kipindi kile ambapo sehemu za burudani na mahoteli yalikuwa yamefungwa walitumia muda huo kukarabati sehemu hizo ili kuziboresha zaidi.

Washikadau hao wamesema kuwa kwa sasa wamegeukia utalii wa ndani kwa ndani sawia na wale wa mataifa jirani ili kuona kwamba wanajiimarisha kiuchumi badala ya kutegemea watalii wa mataifa ya ughaibuni.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.