RUTO AZIDI KUKASHIFIWA NA KINARA WA ODM

Kinara wa ODM, Raila Odinga ameendeleza kashfa zake dhidi ya naibu rais dkt. William Ruto kwa kile alichokisema kuwa anaendeleza siasa za kuwahadaa wananchi pasi na kuwanufaisha kwa namna yoyote.
Akizungumza katika eneo la Dabaso eneo bunge la Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi, Odinga amemkashifu Ruto kwa kile alichodai kuwa amekuwa akihusika katika ubadhirifu wa mali za umma sawia na kesi za ufisadi na kisha kuwahadaa wananchi kupitia misaada ya michango.
Naye mbunge wa suna Mashariki Junet Mohamed ambaye aliambatana na Raila katika ziara yake ya hapa pwani, amemsuta mbunge wa Malindi Aisha Jumwa akidai kuwa hakuna maendeleo yoyote aliyotekelezea wakazi wa Malindi licha ya kukaa uongozini kwa muda sasa.
Akiunga mkono kauli hiyo, katibu msaidizi katika wizara ya ardhi nchini, Gideon Mung’aro amesema kuwa ni wakati sasa viongozi wafisadi wachukuliwe hatua huku akionekana kumtaja Aisha Jumwa kuhusika na kesi za ufisadi.
Naye mbunge wa Mvita kuanti ya Mombasa Abdulswamad Shariff Nassir amesema kuwa kuhamahama kwa vyama vya kisiasa sio suluhu kwa wananchi kupata maendeleo mashinani.
Kwa upande wake seneta mteule kaunti ya Kilifi Christine Zawadi na mwakilishi wa kike Getrude Mbeyu wamemkashifu mbunge wa Malindi kwa kile walichodai kuwa amekuwa akiendekeza siasa za matusi zinazoweza kuwagawanya wananchi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.