Ronaldo ashinda tuzo nyingine kubwa

Cristiano Ronaldo amezidi kujiwekea historia baada ya kutwaa tuzo ya 10 kama mchezaji bora wa mwaka nchini Ureno.

Ronaldo mwenye umri wa miaka 34, amekuwa akifanya vizuri kwenye tuzo hizo tangu mwaka 2007. Huku akiisaidia klabu yake ya Juventus kutwaa taji la nane mfululizo la Serie A.

Nyota huyo ametwaa tuzo hiyo kwa kumshinda kinda wa Atletico Madrid, Joao Felix, mchezaji wa Manchester City, Bernardo Silva, kiungo wa Sporting Lisbon, Bruno Fernandez na Ruben Neves wa Wolves.

Tuzo hizo zimetolewa huko Carlos Lopes Pavilion katika jiji la Lisbon mahala ambapo Ronaldo amekulia wakati alivyokuwa kijana mdogo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.