RIPOTI INAYOHUSIANA NA KIWANDA CHA KOROSHO KAUNTI YA KILIFI YATAKIWA KUHARAKISHWA

Gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ameitaka kamati la bunge la kitaifa kuhusu kilimo, ufugaji na uvuvi kuharakisha ripoti ya inayohusiana na kiwanda cha korosho ambacho kilisambaratika miongo kadhaa iliyopita .
Hii ni baada ya Kingi kusema  ripoti kadhaa zinazofungamana na kufufuliwa kwa kiwanda hicho zimekuwa zikiwasilishwa katika bunge la kitaifa ila hajizaweza kuleta natija yoyote kufikia sasa.
Akizungumza wakati wa kikao na kamati ya bunge la kitaifa iliyozuru kaunti ya Kilifi kutathmini chanzo cha kusambaratika kwa kiwanda  hicho, Kingi amesema kuna idara za serikali ambazo zimekuwa zikisusia kutilia maanani kilimo cha korosho.
Kwa upande wake mwenyikiti wa kamati ya kilimo katika bunge la kitaifa Silas Tiren ambaye pia ni mbunge wa Moiben amesema watahakikisha wanaifanyia kazi kwa haraka ripoti hiyo.
Aidha Tiren amesema ripoti hiyo imecheleweshwa kutokana na bunge kuhairisha vikao mara kwa mara kufuatia maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.