RATIBA YA BAK LEAGUE | SKY HOOPERS KUMENYANA NA GEDE RAPTORS

Michuano ya ligi ya mpira wa kikapu ukanda wa Pwani BAK League inatazamiwa kuendelea wikendi ijayo ya Julai 24, 2021 baada mapumziko wikendi jana.

Kupitia mtandao rasmi wa kijamii wa Twitter uongozi wa BAK League uliweka bayana kuwa mechi hizo – zitakazochezwa katika dimba la Tabernacle Church Watamu, kaunti ya Kilifi – zitaanza kuchezwa kuanzia saa mbili asubuhi na kutamatika saa tisa jioni.

Sky Hoopers watafungua ratiba ya mechi kwa kumenyana na ACK Nets nao Stallions wakivaana na Hamilton Chargers. Vijana wa mji wa Mombasa, Moischer Nets watachuana dhidi ya Kilifi Spurs. Gede Raptors watafunga ratiba ya mechi za asubuhi kwa kuvaana dhidi ya Millenium Ballers.

Raundi ya pili imepangwa kuanza saa nane mchana ambapo ACK Nets watachuana dhidi ya Moischer Nets huku Sky Hoopers wakipimana nguvu baina ya Gede Raptors.

Mechi ya Millennium Ballers  dhidi ya Stallions imepangwa kuchezwa saa nane mchana nao Hamilton Chargers wakimaliza udhia dhidi ya Kilifi Spurs.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.