RAIS WA POLAND AMKABIDHI TUZO YA HAIBA KUBWA MCHAWI WA MAGOLI, ROBERT LEWANDOWSKI

Rais wa taifa la Poland, Andrzej Duda, amemkabidhi mchawi wa magoli Robert Lewandowski, tuzo ya haiba kubwa ya Commander’s Cross of the Order of Polonia Restituta kutokana na ukubwa na upekee wa mchango wake katika ulingo wa soka akichezea Bayern Munich ya Ujerumani na timu ya taifa ya Poland.

Tuzo hiyo huwa maalumu kwa maafisa wa jeshi na raia wa kawaida wanaodhihirisha matendo bora ya kuipa jamii mwelekeo mwema nchini Poland. Lewandowski, 32, ni mtu wa tatu baada ya aliyekuwa Rais wa Poland, Lech Walesa na Rais wa zamani wa Amerika, Dwight D. Eisenhower kuwahi kupokea tuzo hiyo.

Taji hilo linaongeza idadi ya mataji katika kabati la Lewandowski ambaye tayari amejivunia makombe mbalimbali chini ya kipindi cha msimu mmoja na nusu uliopita.

Lewandowski alituzwa mahsusi kutokana na mchango wake katika kampeni za msimu wa 2019-20 ambapo alitia kapuni mataji ya Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), DFB-Pokal (German Cup) na Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Nyota huyo aliibuka mfungaji bora katika kila mojawapo ya mapambano hayo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.