RAIS UHURU KENYATTA AZURU KAMBI YA WANAMAJI YA MANDA

Kikosi cha jeshi la Wanamaji nchini katika kambi ya Manda Bay kaunti ya Lamu kimepongezwa na rais Uhuru Kenyatta kwa kuwa imara katika kudumisha usalama wa nchi.
Rais amesema kikosi hicho kimekuwa kikitia juhudi kuhakikisha usalama unaboreshwa vilivyo hasa kwenye mpaka wa Kenya na Somali pamoja na baharini.
Kenyatta akizungumza katika hafla ya kupandisha hadhi kambi ya jeshi la Wanamaji ya Manda amewataka kuendelea kudumisha usalama nchini akisema atahakikisha anawapatia raslimali na vifaa ambavyo wanahitaji ili kuzidi kulinda taifa hili.
Aidha rais ametoa wito kwa wenyeji pamoja na viongozi katika kaunti hiyo kushirikiana na asasi za usalama ili kudumisha usalama kwenye kaunti hiyo na nchini kote kutokana na miradi ya maendeleo ambayo inawekezwa kwenye kaunti hiyo..
Katika kambi hiyo Rais Kenyatta amefungua mradi wa hospitali Trauma Centre ambayo itawahudumia wanajeshi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.