RAIS KENYATTA AZINDUA DARAJA JIPYA LA MIGUU ENEO LA LIWATONI KAUNTI MOMBASA

Rais Uhuru Kenyatta amezindua Rasmi daraja jipya la miguu ambalo linaunganisha kisiwa cha Mombasa na Likoni eneo la Liwatoni kaunti ya Mombasa.
Katika uzinduzi huo rais Uhuru Kenyatta amewahimiza wenyeji wa kaunti hiyo kuwa na subira hadi mwezi Januari mwaka ujao wa 2021 ili waweze kutumia daraja hilo.
Katika taarifa yake alipokuwa anazindua daraja hilo Rais amehoji kuwa hii ni kwa misingi kuwa usalama wa wananchi ambao wanatumia kivuko hicho kwamba ni lazima uzingatiwe kwa kina hivyo kuwapa wahandisi waliopewa kandarasi hiyo ya hadi mwishoni mwa mwezi huu wa Disemba kuhakikisha kila kitu kiko tayari kufuatia usalama wa watakaotumia daraja hilo.
Wakati uo huo Gavana wa kaunti ya Mombasa Ali Hassan Joho amempongeza rais Kenyatta kufuatia juhudi za kuhakikisha kuwa mpango huo unatimia na kusema litakuwa lenye manufaa mengi kwa wenyeji kwa taifa la Kenya kwa ujumla na kuongeza kuwa utapunguza msongamano katika kivuko cha Likoni.
Ni mradi ambao umegharimu kima cha shilingi bilioni 1.9.

1 thought on “RAIS KENYATTA AZINDUA DARAJA JIPYA LA MIGUU ENEO LA LIWATONI KAUNTI MOMBASA”

  1. Hongera Sana Kwa Mheshimiwa Rais!Kivuko Hicho Cha Daraja Kitarahisisha Kazi Ya Usafiri Na Kupunguza Msongamano Baina Ya Wasafiri

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.