POGBA KUYOYOMEA PSG

Mino Raiola wakala wa nyota wa Manchester United, Paul Pogba, yupo kwenye majadiliano na klabu inayoshiriki Ligue 1, Paris Saint-Germain kwa ajili ya usajili wa mteja wake huyo huku wakimtaka kwa pauni milioni 43.

Pogba amebaki na mkataba wa mwaka mmoja ndani ya Man United na bado hajafanya mazungumzo na klabu yake ya sasa.

Si mara ya kwanza kwa kiungo huyo kutaka kuondoka ndani ya United na safari hii huenda akaondoka kikosini hapo.

PSG wanaamini kuwa wanaweza kumpata Pogba kwa pauni 43m ndiyo maana imeelezwa kuwa kwa sasa hivi wako kwenye mpango wa kuwauza baadhi ya nyota wa kikosi hicho ilikuweza kupata pauni 50m za usajili wake.

Taarifa zinaeleza kuwa PSG wanaomba kupunguziwa bei katika kumpata nyota huyo wa Man United.

Hata hivyo, Man United awali ilieza kuwa nyota wake huyo watafanya naye mazungumzo baada ya michuano ya Euro 2020 kwa ajili ya mkataba mpya, lakini mpaka sasa kumekuwa kimya na haijafahamika kama atasalia hapo au ataondoka.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.