Pep Guardiola asema pengo ni kubwa ila bado anaamini timu yake inaweza kuifikia Liverpool

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola anasema “pengo ni kubwa” lakini bado anaamini timu yake inaweza kuifikia Liverpool katika kinyang’anyiro cha kuwania taji la ligi kuu England.

Pigo la Wolves 2-0 dhidi ya City ina maana sasa klabu hiyo ipo nyuma kwa pointi nane nyuma ya Liverpool.

Ni tofauti kubwa iliyowahi kuwepo baada ya mechi nane katika ligi kuu ya England, Timu ya awali iliyowahi kuwa katika nafasi hiyo ni Chelsea mnamo 2014, iliyoishia kushinda taji.

Kushindwa huko kuna maanisha kuwa City inakabiliwa na mwanzo mbaya kuwahi kushuhudiwa tangu kampeni ya 2013-14 chini ya Manuel Pellegrini, wakati waliposogea na kushinda taji.

Kabla ya mechi dhidi ya Wolves, City ilikuwa ndio timu kati ya ‘sita kubwa’ ‘ambayo Wolves ilishindwa kuifunga tagu kuanza kwa msimu, ikiwa imezifunga nyingine kwenye ligi na kuwahi kuiondoa Liverpool kwenye kombe la FA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.