OWEN BAYA ATAKA UCHUNGUZI KUFANYWA KUHUSIANA NA WIZI ULIOFANYIKA KWENYE KIWANDA CHA KOROSHO

Mbunge wa Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi Owen Baya anaitaka kamati ya bunge la kitaifa kuhusu kilimo, ufugaji na uvuvi kufanya uchunguzi kuhusiana na wizi uliofanyika katika kiwanda cha korosho miaka mingi iliyopitia.
Kulingana na Baya kiwanda hicho ambacho kilianzishwa mwaka wa 1975 kiliuzwa na watu binafsi baada ya kuchukua mkopo kutoka kwa benki moja nchini.
Akizungumza mjini Kilifi mbele ya kamati ya bunge kuhusu kilimo ambayo inapokea maoni kutoka kwa wakazi kuhusu kilimo Cha korosho ,Baya amesema baada ya kiwanda hicho kufungwa wakazi wengi wamesalia kuwa masikini kaunti ya Kilifi kwa sababu walikuwa wametegemea korosho.
Baya amesema kuwa kiwanda hicho pia kilikuwa kigezo kikuu cha kukuza uchumi wa kaunti ya Kilifi na pwani kwa jumla hivyo kuna haja ya kiwanda hicho kurejelea shughuli zake kama hapo awali.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.