OLYMPAFRIKA KUJENGA UWANJA NCHINI KENYA

Wanariadha raia wa Kenya wanakila sababu za kutabasamu baada ya ujenzi wa kituo cha kisasa cha kukuza talanta cha OlympAfrica katika uwanja wa Muhuri Muchiri mtaani Ruai katika kaunti ndogo ya Kasarani jijini Nairobi, Kenya, kutajwa kuanza miezi mitatu ijayo.

Kituo hicho ni matunda ya mkataba kati ya Kamati ya Taifa ya Olimpiki Kenya (NOC-K), mfuko wa OlympAfrica na serikali ya Kaunti ya Nairobi.

Ndoto ya Kenya kuwa taifa la 38 barani Afrika kuwa na kituo cha chipukizi cha OlympAfrica ilianza kuchukua mwelekeo mzuri Jumatano baada ya Kaunti ya Nairobi kuipatia rasmi NOC-K shamba la ekari 10 ambalo ilikuwa imeahidi kwa ujenzi wa kituo hicho.

Kaimu Gavana wa Nairobi, Ann Kananu na rais wa NOC-K Paul Tergat, ambaye alikuwa ameandamana na meneja wa miradi ya OlympAfrica, Yaye Ndiate Sall walisaini mkataba ambao sasa umeidhinisha ujenzi wa kituo hicho uanze.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.