NCCK YAWATAKA VIJANA KANDA YA PWANI KUJIEPUSHA NA WANASIASA WANAOPANIA KUWATUMIA VISIVYO

Katibu mkuu wa baraza la kitaifa la makanisa nchini NCCK Chris Kinyanjui amewahimiza vijana kanda ya pwani kujiepusha na wanasiasa ambao wanapania kuwatumia visivyo kuzua vurugu kabla na baada ya uchaguzi.
Kinyanjui amesema kuwa baraza hilo limeanzisha hamasa kwa vijana kuhusu umuhimu wa kudumisha amani nchini.
Aidha amesema ni jukumu la kila mmoja kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani katika taifa hili.
Haya yanajiri huku mwenyekiti wa baraza hilo kanda ya Pwani Askofu Daktari Peter Mweru akisema hakuna mwanasiasa ambaye ataruhusiwa kuendeleza siasa katika maeneo ya ibada.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.