NAIBU WA RAIS AWAPUZILIA MBALI WANAOKOSOA HATUA YAKE YA KUTOA FEDHA ZA KUCHANGISHIA MIRADI

Wanasiasa mbalimbali nchini wanapoendeleza kampeni zao kwa ajili ya maandalizi ya uchaguzi mkuu ujao wa 2022 naibu wa Rais Daktari William Samoei Ruto amewapuzilia mbali wapinzani wake wa kisiasa ambao wanakosoa hatua yake ya kutoa fedha za kuchangishia miradi ya maendeleo kanisani.
Ruto akizungumza katika kanisa la Redeemed Gospel wadi ya Mikindani eneo bunge la Jomvu kaunti ya Mombasa ameahidi kushirikiana na viongozi hao wa makanisa huku akisema wapinzani wake hawatamzuia kutoa misaada.
Aidha, amewaomba viongozi wa dini kuliombea taifa la Kenya linapojiandaa kwa uchaguzi mkuu ujao wa 2022.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.