NAIBU GAVANA WA TAITA TAVETA ASEMA JUHUDI ZINAWEKWA KUIMARISHA HUDUMA ZA AFYA

Naibu gavana wa kaunti ya Taita Taveta Christine Kilalo amesema serikali ya kaunti hiyo itaweka juhudi kuhakikisha kuna madawa ya kutosha kwenye hospitali na zahanati za umma katika kaunti hiyo.

Kilalo amesema suala la uhaba wa madawa limekuwa likiwakabiliwa wenyeji hasa kwenye zahanati zilizoko mashinani.

Amesema wanashirikiana na KEMSA kuhakikisha usambazaji wa madawa unafanyika kila wakati ili wenyeji wapate huduma bora za matibabu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *