MWINYI MWASERA ADAI MATUGA IMETENGWA KWENYE MIRADI YA MAENDELEO

Eneo bunge la Matuga kaunti ya Kwale linadaiwa kutengwa katika miradi ya maendeleo ya kampuni ya uchimbaji madini ya Base Titanium.
Akitoa lalama hizo mwakilishi wa wadi ya Waa Ng’ombeni Mwinyi Mwasera anadai kuwa Matuga imetengwa baada ya kukosa kujumuishwa katika kamati ya maendeleo ya jamii zilizoathirika na shughuli za uchimbaji wa Madini.
Aidha amesema kuwa mikakati imeanzishwa kuhakikisha eneo bunge hilo linafaidika na miradi ya maendeleo ya jamii kutoka kwa kampuni hiyo ya uchimbaji Madini.
Naye Mshenga Ruga ambaye ni mwenyekiti wa kamati hiyo katika eneo bunge la Msambweni akizungumza huko Waa amesema Matuga ina haki ya kunufaika na miradi hiyo ili kuwafaidi wenyeji na kuitaja Matuga kama baadhi ya maeneo ambayo yameathirika na shughuli za uchimbaji madini katika kaunti hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.