Mwili wapatikana kichakani ukiwa umeoza eneo la Mwangani, Kilifi

Asasi za usalama zimeanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha jamaa mmoja ambaye mwili wake umepatikana leo kwenye kichaka ukiwa umeoza eneo la Mwangani kaunti ya Kilifi.
Kulingana na mzee wa Kijiji wa eneo Hilo Safari Kadenge ni kwamba marehemu kwa jina Kadzomba Kahindi alitoweka Siku sita zilizopita kabla ya kupatikana leo akiwa ameaga dunia.
Mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 35 amepatikana akiwa na kipande cha leso shingoni hali ambayo inadaiwa huenda alijitoa uhai kwa kujitia kitanzi.
Chanzo cha kifo hicho hakijabainika hadi kufikia sasa huku akiacha mjane mmoja na watoto wanne na mwili wake umechukuliwa na maafisa wa polisi na kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya kaunti ndogo ya Malindi.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.