MWENDWA APATA UHURU. MAHAKAMA YASEMA HANA HATIA

Rais wa shirikisho la soka FKF humu nchini Nick Mwendwa hana hatia  baada ya mahakama kufunga faili yake bila kumfungulia mashtaka yoyote.

Mahakama imeagiza kuwa kuwa fedha alizokuwa ametoa kama dhamana ambazo ni kima cha shilingi milioni 4 zirejeshwe.

Hii ni baada ya muda wa makataa ya siku saba aliyotoa hakimu Wandia Nyamu  kuwasilisha kesi dhidi ya Nick Mwendwa aliyeng’atuliwa la sivyo mahakama itupilie mbali kesi hiyo.

Mwendwa alikuwa anazuiliwa na maafisa wa polisi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha  takriban  shilingi milioni 500 zilizotoka kwa wizara ya michezo kusimamia masuala ya soka.

Waziri wa michezo Balozi Amina Mohamed alivunjilia mbali shirikisho la soka la FKF na kuteuwa kamati iliyopewa jukumu la kusimamia masuala ya soka kwa muda.

Mwendwa alikuwa amepewa masharti na mahakama ya kutojihusisha na shughuli zozote za michezo na kutofika katika ofisi za FKF ili kupisha nafasi ya uchunguzi kuhusiana na hela zilizofujwa utamatike.

Ligi zote za kitaifa zilikuwa zimesitishwa kwa muda wa wiki mbili na kamati teule  inayoongozwa na jajim mstaafu Aaron Ringera.

Kwa mujibu wa maafisa wa FIFA ni kuwa  Kenya huenda ikapigwa marufuku ya soka kwa sababu kamati iliyobuniwa na wizara ilikuwa kinyume na sheria za FIFA pamoja na serikali kuingilia masuala ya FKF iliyochini ya FIFA.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.