KUUNGANISHWA KWA MASHIRIKA YA KPA, KENYA FERRY NA KENYA PIPELINE YADAIWA HAYATAATHIRI SHUGHULI ZA UCHUKUZIHUKUZI INCHINI

Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa kuhusu fedha na mipango Gladys Wanga amehoji kuunganishwa kwa mashirika matatu ya uchukuzi wa umma ikiwemo KPA, Shirika la Ferry Nchini na Kenya Pipeline hakutahitilafiana na shuguli za uchukuzi hapa nchini.
Akizungumza huko Mombasa amesema kuunganishwa kwa sekta hizo tatu kutasaidia katika kuboresha shughuli za uchukuzi nchini sambamba na kimataifa.
Hata hivyo amewataka wanaopinga mchakato huo kuondoa hofu kwani hakuna ajira au uchumi utakaoathirika na hatua hiyo.
Wakati uo huo mbunge wa Lamu Magharibi ambaye ni mwanachama wa kamati hiyo Stanley Muthama amesema kwa mujibu wa maelezo ambayo kamati hiyo imepata ni kuwa shuguli za uchukuzi zitaimarishwa kupitia mbinu ya kuunganishwa kwa mashirika hayo matatu.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.