Muimbaji wa injili Mr Seed kuachia wimbo mpya siku chache baada ya kuwa baba

Muimbaji wa nyimbo za injili Mr.seed anapania kuachia wimbo mpya [UPO] wiki hii akimshirikisha Solomon Mkubwa, siku chache baada ya kuwa baba.
 
“Wimbo ni kuhusu shukrani kama njia ya kumregeshea shukrani mwenyezi Mungu kwa ukuu wake pamoja na yale ambayo anayafanya maishani mwangu, ” amesema Mr. Seed.
 
Wimbo huu unakuja siku chache tu baada ya mke wake, Nimo Gachuiri, kujifungua mtoto wa kiume na kumpa jina la Gold Christen.
 
Upo utakuwa wimbo wa pili baada ya baba Christen kutoka EMB record label inayomilikiwa na Bahati.
 
Mr Seed amesema kwamba anafuraha kuwa nje ya EMB na familia yake ipo vizuri. “Ni jambo la furaha kuwa mme wa mtu na baba wa mtu hasa siku hizi ambazo sasa nafaa kujua kubadilisha nepi mtoto, ” amesema Seed.

 

https://www.instagram.com/p/BvJCfP_Fo9t/

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.