MSAKO DHIDI YA UUZAJI WA POMBE HARAMU WAANZISHWA MOMBASA

Msako dhidi ya uuzaji wa pombe haramu kaunti ya Mombasa umezinduliwa na mshirikishi mkuu wa utawala kanda ya pwani John Elungata.
Katika uzinduzi huo Elungata amesema ni msako ambao utaendelezwa kwa muda wa siku 30 na kuwataka wenyeji wa kaunti ya Mombasa kushirikiana na kamati maalum ambayo inaendeleza oparesheni hiyo kwa kuwaripoti wauzaji wa pombe haramu.
Amesema msako huo utasaidia kudhibiti uuzaji wa pombe ambayo haijafikia kiwango hitajika kwa mujibu wa mamlaka ya kutathmini ubora wa bidhaa nchini KEBS.
Naye Gilbert Kitiyo ambaye ni kamishna wa kaunti hiyo amesema msako huo utachangia kwa kiwango kikubwa kupunguza kwa visa vya uhalifu katika kaunti ya Mombasa.
Naye George Karisa ambaye ni afisa wa kupambana na mihadarati na vileo haramu nchini NACADA kanda ya pwani amesema oparesheni hiyo itafanikiwa kwa kuwa wameshirikiana na viongozi walioko mashinani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.