Mombasa | Zoezi la kutafuta miili katika kivuko cha Likoni kuendelea leo

Mkuu wa jeshi la wanamaji Lawrence Gituma anaongoza zoezi la kusaka miili katika kivuko cha Feri cha Likoni kaunti ya Mombasa leo ikiwa ni siku ya nne tangu kuanza kwa shughuli hiyo.

Hadi kufikia sasa jumla ya maeneo 6 ambayo yalikuwa miongoni mwa sehemu zilizodaiwa huenda gari lililozama likiwa na watu hao katika kivuko hicho lilikwama yamefanyiwa ukaguzi na wapiga mbizi ambao wanaongozwa na jeshi la wana maji.

Msemaji wa serikali kanali mstaafu Cyrus Oguna amesema wapiga mbizi wataendelea kuyakagua maeno mengine 8 ambayo yamesalia.

Hata hivyo amesema ana matumaini kuwa eneo ambalo gari hilo limekwama kupatikana na ikiwa ukaguzi katika maeneo hayo yatakamilika bila kupatikana mikakati zaidi itawekwa ili kuendelea kulitafuta.

Kwa upande wake mbunge wa Likoni Mishi Mboko amewahimiza maafisa wanaoongoza zoezi la kusaka miili hiyo kushirikiana ili kufanikisha shughuli hiyo na kusema ukosefu wa ushirikiano baina ya vikosi hivyo ni kati ya changamoto ambazo zinazikumba oparesheni hiyo.
Ameahidi kuwa serikali inajitahidi kuhakikisha miili hiyo inapatikana.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.