Mombasa | Wapiga mbizi kutoka Afrika Kusini wawasili Likoni kusaka miili iliyozama

Shughuli ya kusaka miili ya mama na mwanawe waliozama katika bahari Hindi mjini Mombasa katika kivuko cha Likoni Feri imerejelewa muda mfupi baada ya kusitishwa kwa muda ili kuzipa fursa meli za kijeshi kutoka India kutua nanga.

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa huduma za Feri, Dan Mwazo, ni kwamba shughuli hiyo kwa sasa inaendeshwa kwa mitambo ya kidijitali.

Aidha mwazo anasema wapiga mbizi kutoka Afrika Kusini waliokodishwa na familia ya Mariam Kighenda na mtoto Amanda Mutheu wamewasili. Wapiga mbizi hawa watashirikiana na kikosi cha wanamaji wa Kenya katika oparesheni ya kuwaska wawili hao ambao imeingia siku ya 9 leo.

Mkasa huo umevutia hisia za huzuni kutoka kwa watu katika pembe zote za dunia, huku kukiwa na manung’uniko kwamba vitengo vya uokozi vilichelewa mno kuokoa  Bi Mariam Kighenda na mwanawe Amanda Mutheu.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.