Mombasa | Wanaowakodishia vyumba wanafunzi Mombasa kuchunguzwa

Imebainika kuwa kuna baadhi ya wanafunzi katika kaunti ya Mombasa wanaokodi vyumba ili kufanya ngono punde tu wanapotoka shuleni.

Haya yanajiri huku wito ukitolewa kwa asasi za usalama kaunti hiyo kuwafuatilia wamiliki wa nyumba za makazi ambao wanawaruhusu wanafunzi kukodi vyumba hivyo na kuhakikisha tabia hiyo inakomesha mapema iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa baadhi ya wakazi wa Chaani katika kaunti hiyo wanasema kuwa kuna wanafunzi wa shule za upili na wa msingi ambao wamekuwa wakikodi vyumba vya kulala eneo la Changamwe kaunti hiyo ya Mombasa ili kushiriki ngono.

Wakati uo huo naibu mwenyekiti mwenyekiti wa chama cha walimu KNUT tawi la Kilindini Ahmed Kombo Ahmed amesema kuwa hatua za kishera zinapaswa kuchukuliwa dhidi ya wamiliki wa vyumba hivyo ambao wanawakodishia wanafunzi hao nyumba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.