Mombasa | Walanguzi wa dawa za kulevya kikaangoni

‘Wafanyibiashara wa ulanguzi wa dawa za kulevya katika kaunti ya Mombasa hawatasazwa.’ Ni kauli ya kamanda wa polisi kaunti ya Mombasa Johnstone Ipara ambaye amesema msako wa kiusalama utawalenga walanguzi wote wa dawa za kulevya wanaojihusisha na biashara hiyo.

Ameyasema oparesheni hiyo inapania kuwalenga walanguzi wakuu kama njia mojawapo ya kulinda kizazi kichanga katika kaunti ya Mombasa.

Ametaja kuzinduliwa kwa vituo vya polisi kama kile cha Kadzandani na Mwatamba eneo bunge la Kisauni na Junda vitasaidia katika kukabiliana na utovu wa usalama katika kaunti hiyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.