Mombasa | Polisi kuchunguza kifo cha mwanafunzi aliyeanguka kutoka kwa jengo la ghorofani

Polisi katika kaunti ya Mombasa wameanzisha uchunguzi kufuatia kifo cha mwanafunzi mmoja aliyeripotiwa kuanguka kutoka kwenye ghorofa moja kule Mshomoroni katika eneo la mwisho wa lami kaunti ya Mombasa alipokua akizungumza kwa kuptia simu ya mkononi.

Akidhibitisha kisa hicho kamanda wa polisi eneo la Kisauni,Julius Kiragu amesema kwamba Edwin Kibet ambaye alikuwa akisomea utabibu katika mwaka wake wa tatu kwenye chuo kikuu cha Mombasa Techinical TUM alianguaka na kugongwa na vyuma hali iliyopelekea yeye kujeruhiwa vibaya yaliyopelekea kifo chake.

alisema kwamba mwanafunzi huyo ambaye anasomea udaktari wa kliniki alikua mwaka wa tatu na alipokua akianguka aligongwa na vyuma jambo ambalo lilimpea majeraha mwilini na kupelekea kifo chake.

Kulingana na walioshuhudia kisa hicho ni kwamba,Edwin aliyekua akikaa na mlezi wake,Rashid Kibet alitoka nje ya nyumba muda wa saa tisa asubuhi na kupanda ghorofa ya nne ili kupokea simu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.