Mombasa | Mbunge ayataka mashirika ya akiba na mikopo kusaidia jamii

Mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir amesema mashirika ya akiba na mikopo miongoni mwa kina mama kaunti ya Mombsa yameleta ufanisi mkubwa.

Kwenye hotuba yake akiwa katika kaunti hiyo mbunge huyo sasa ameyataka mashirika hayo kuwa na ushirikiano ili kusaidia kubuni miradi mbali mbali ambayo itasaidia watu kujiendeleza maishani.

Abdulswamad ametoa wito kwa mashirika hayo kubuni shirika kubwa ambalo litasaidia kuwakilisha kaunti hiyo ya Mombasa kama njia mojawapo ya kuinua kina mama wanaoishi mashinani.

Ameongezea kuwa ataishinikiza bunge kupitisha hoja ya kuwasaidia kina mama katika mashirika tofauti ya akiba na mikopo ili kuwasaidia kujiendeleza katika maisha yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.