Mombasa | Mbunge Abdulswamad Nassir atoa pendekezo la kufungwa kwa akaunti za benki

Pendekezo la kufungwa kwa akaunti zote za benki za washukiwa wa ulanguzi wa dawa za kulevya limetolewa na mbunge wa Mvita Abdulswamad Shariff Nassir.

Sheriff amesema kuwa hatua ya kuwaruhusu washukiwa kuweka fedha zao kwenye akaunti za benki na kuendeleza biashara hiyo ya dawa za kulevya haistahili na kusema mali yao pia inafaa kutwaliwa na serikali na uchunguzi wa kina kuanzishwa mara moja dhidi yao.

Wakati uo huo aliyekuwa mgombea wa kiti cha ugavana katika kaunti ya Mombasa Suleiman Shabaal amehoji biashara ya dawa za kulevya imeathiri vijana wengi pwani hivyo basi ni vyema kwa wahusika kuchukuliwa hatua hitajika kwa mujibu wa sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.