Mombasa | Kaunti yatenga Ksh 35M kutoa elimu ya Blue Economy kwa vijana Mombasa

Kima cha shilingi milioni 35 zimetengwa na serikali ya kaunti ya Mombasa kuwasaidia vijana wa kaunti hiyo kupata mafunzo ya uchumi wa baharini kwa maana ya Blue Economy.

Haya ni kulingana na waziri wa maswala ya vijana, jinsia na michezo katika serikali ya kaunti hiyo Munywoki Kyalo ambaye amesema vijana wanapaswa kujitokeza kwa wingi ili kufaidi na mpango huo.

Akizungumza katika kaunti ya Mombasa amesema serikali ya kunti hiyo inapania kuanzisha kitengo maalum ambacho kitawasaidia vijana kujiunga na mpango huo kila panapotokea nafasi za ajira.

Kulingana na waziri huyo kwa sasa serikali ya kaunti ya Mombasa imetenga kima cha shilingi milioni 100 kuwasaidia vijana ambao walimaliza masomo yao ya shule ya upili ili kuendeleza masomo yao katika vyuo vya kiufundi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.