Mombasa | Naibu Kamishna wa Changamwe ataka ushirikiano miongoni mwa viongozi katika zoezi la Sensa

Shule zote zinapotarajiwa kufunguliwa rasmi tarehe 2 mwezi wa Septemba mwaka huu kwa muhula wa tatu ili kuzuia wazazi kusafiri na watoto wao usiku wa tarehe 24 na 25 wakati zoezi la sensa litakapokuwa linaendelea kote nchini, naibu kaunti kamishna eneo bunge la Changamwe kaunti ya Mombasa Tom Wevi Konyelo amelitaja zoezi hilo kuwa la umuhimu mkubwa kwa taifa hili.

Amesema zoezi hilo huwa linasaidia serikali kupata takwimu kuhusu idadi ya wanaozaliwa au kuaga dunia na ukuaji wa idadi ya watu, hivyo kupangia utoaji huduma mbalimbali nchini.

Amewataka machifu na manaibu wao kushirikiana vyema na wazee wa mitaa kuhamasisha wananchi kuhusu zoezi hilo na pia kutoa habari kwa asasi za usalama kuhusu yeyote mwenye nia ya kutatiza zoezi hilo.

Shughuli hiyo imeungwa mkono na Mbunge wa changamwe Omar Mwinyi na Badi Twalib wa Jomvu na kuwasihi wakazi kusalia majumbani mwao ili kuhesabiwa usiku wa tarehe 24/25.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.