MOHAMED MWACHAUSA AITAKA IDARA YA USALAMA KUIMARISHA DORIA KWALE

Shirika la kijamii la Samba Sports Youth Agenda limeitaka idara ya usalama kaunti ya Kwale kuimarisha usalama kabla, wakati na baada ya kuandaliwa kwa kipute cha uchaguzi mkuu wa Agosti 9 mwaka huu wa 2022.
Mshirikishi wa shirika hilo Mohammed Mwachausa amesema hatua hiyo itazuia visa vya utovu wa usalama na machafuko baada ya uchaguzi.
Akizungumza na wanahabari, Mwachausa amevitaka vitengo vya usalama kuwakabili wale wanaolenga kuzua vurugu.
Kwa upande wake kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amesema tayari idara ya usalama kaunti hiyo imejiandaa vilivyo ili kuzuia vurugu kabla, wakati na baada ya uchaguzi wa Agosti 9 na kuwataka wananchi kushirikiana na asasi za usalama ili kuhakikisha uchaguzi huo unafanyika kwa amani.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.