Mkenya kinda asajiliwa na klabu ya Uingereza

Huku ndoto za nguli wa soka raia wa Tanzania, Mbwana Samatta, zikiangukia pua, mkenya Clarke Sydney Omondi Oduor aliibuka miongoni mwa wanasoka wawili walionaswa na Barnsley FC ya Uingereza siku moja kabla ya kukamilika kwa kipindi cha uhamisho.

Chipukizi huyo alisajiliwa wakati mmoja na Patrick Schmidt raia wa Australia.

Usajili huo unatoa nafasi kwa chipukizi huyo kuorodheshwa miongoni mwa wasajili wapya 12 watakaosakata kabumbu katika klabu hiyo muhula huu.

Oduor mwenye umri wa miaka 20 tayari ametia wino kandarasi ya miaka minne kusakatia klabu hiyo kwenye kampeni za soka la daraja ya pili akitokea Leeds United ambayo pia hushiriki kipute hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.