MIUNDO MSINGI DUNI, CHANZO CHA WACHEZAJI PWANI KUKOSEKANA HARAMBEE STARS

Swala la ukosefu wa miundo msingi bora katika sekta ya michezo eneo la pwani ndicho chanzo kikuu cha wachezaji kutoka pwani kutochaguliwa kuchezea timu ya taifa nchini, Harambee Stars.

Ni usemi wake mwenyekiti wa shirikisho la soka kaunti ya Kilifi Dickson Angore ambaye amesema mara nyingi wakufunzi wa timu ya taifa wanaangalia mchezaji aliyehitimu na mzoefu.

Angore pia amesema Shirikisho hilo linahimiza wakufunzi katika eneo hili la Pwani kusoma ili kuwapa wachezaji mwelekeo unaostahili.

Aidha mwenyekiti huyo amewataka washikadau wa michezo kutafuta mbinu mbadala kusaidia vijana kipindi hiki cha Corona na hususan wanapowazia swala la kufungia michezo.

Ameongezea kuwa swala la kusitishwa kwa michezo eneo hili limekuwa pigo sio tu kwa vijana lakini pia kwa shirikisho kwa kile alichokitaja kama athari ya kushushwa daraja kwa vilabu kufuatia kutotii ratiba za mechi.

 

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.