MIUNDO MISINGI DUNI YA ATHIRI BIASHARA ENEO LA MALINDI KAUNTI YA KILIFI.

Wafanyibiashara hapa mjini malindi wanalalamikia miundo msingi duni hali inayowaathiri kibiashara.

Wafanyibiashra hao wamesema kuwa tangia kuanza kushuhudiwa mvua katika mji huu, maji ya mvua yamekuwa yakitapakaa katika maeneo ya kibiashara jambo linalozuia wateja wao kumiminika kwa wingi katika biashara hizo.

Wamesema kuwa mipangilio ya mji huu wa malindi ni duni mno ndiposa maji hutapakaa hata katika barabara za mji huu wakati ambapo kunashuhudiwa mvua.

Wameitaka serikali ya kaunti ya Kilifi sawia na ile ya kitaifa kuhakikisha kuwa zinashirikiana ili kuona kwamba hali ya miundo msingi inaimarishwa ikizingatiwa kwamba Malindi ni mji wa kitalii.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.