MISHI MBIKO AWATAKA WENYEJI WA MOMBASA KUMUUNGA MKONO ABDULSWAMAD SHARIF NASSIR

Mbunge wa Likoni kaunti ya Mombasa Mishi Juma Mboko amewarai wenyeji kumchagua kiongozi ambaye atawatekelezea miradi ya maendeleo.
Mishi ambaye anaunga mkono azima ya mbunge wa Mvita Abdulswamad Sharif Nassir kuwania wadhifa wa ugavana katika kaunti hiyo amewarai wenyeji kumchagua kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2022 na kumtaja kama kiongozi ambaye anapaswa kumrithi gavana Ali Hassan Joho.
Amesema mbunge wa Mvita ametekeleza miradi mingi ya maendeleo katika eneo bunge lake na hata kuwatetea wapwani bungeni hivyo anastahili kuwaongoza wenyeji wa Mombasa kama Gavana.
Ni kauli ambayo imesisitizwa na mwakilishi wa wadi ya Timbwani Mwaka Bakari ambaye amewahimiza wakazi kumchagua mbunge huyo wa Mvita..
Haya yanajiri huku wadhifa wa ugavana katika kaunti hiyo ukimezewa mate na wengi akiwemo mwanabiashara Suleiman Shahbal , mbunge wa Kisauni Ali Menza Mbogo na naibu wa gavana kaunti ya Mombasa Daktari William Kingi miongoni mwa viongozi wengine.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *

SUBSCRIBE TO OUR E- NEWSLETTER

Subscribe to our mailing list and get interesting stuff and updates to your email inbox.